Simba SC weka mbali na watoto

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC unaweza kusema weka mbali na watoto, baada ya usiku huu kuifunga Coastal Union ya Yanga mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Meja Isamuyo Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mabao yote ya Simba SC yamepatikana kipindi cha kwanza yakiwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Seleman Mwalimu dakika ya 25 goli ambalo linaonekana kuwa bora wakati bao lingine limefungwa na beki wa kati Ismail Toure dakika ya 45.

Kwa matokeo hayo Simba SC sasa imefikisha pointi 34 ikiwa imecheza mechi 15 ikiwashusha Azam FC kwenye nafasi ya pili huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons