Simba bado wanazitaka pointi 3 za Damaro

Ni kama bado wanazitaka pointi 3 za chee kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga SC kwa kitendo chao cha kumtumia mchezaji wao Mohamed Damaro ambaye uraia wake wa Tanzania haujakamilika.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC Crescentius Magori ameendelea kukazia mpango wao wa kutaka wapewe pointi 3 licha kwamba madai yao yalitupiliwa mbali na TFF.

"Mwaka jana na sisi tuliandika barua ya kubadili uraia wa wachezaji wetu lakini haijajibiwa hadi leo. Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa haipo kwenye mizania sawa sio japo sawa. Hili japo sio tu tunakwenda CAS lakini pia tunaiandikia FIFA. Kama mtu anapewa uraia ili tu achezee klabu pekee bila timu ya taifa ni jambo ambalo halikubaliki. Damaro hata ipite miaka 100 hawezi kucheza timu ya Taifa. Jambo lingine ambalo TFF walitakiwa walifanye, kama kanuni zetu halizungumzii hilo basi wangetumia kanuni za juu kufanya maamuzi."

"Hili jambo sio fair sababu kuna timu moja ina wachezaji 13 kwa kutumia mlango wa nyuma. Na aliyedanganya mamlaka kwamba anapewa uraia ili acheze timu ya taifa basi alifanya udanganyifu mkubwa, unampa uraia wa nini tena mchezaji mwenyewe hana hata mwaka Tanzania. Ni jambo serious na sisi tupo nalo serious."

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenziya Simba, Crescentius Magori.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons