Sakata la Damaro, lamuibua Samuel Eto' o

Samuel Eto'o alipata uraia wa Hispania mnamo Oktoba 17, 2006, wakati akiwa mchezaji wa Barcelona.

Hii ilimruhusu kucheza kama mchezaji wa Ulaya, na kumfaa katika mashindano ya klabu za Ulaya.

Na kwa mujibu wa katiba ya Cameroon nchi hiyo hairuhusu uraia pacha.

Lakini Eto'o alipata uraia wa Hispania na kuendelea kuitumikia Cameroon na leo hii ni rais wa Shirikisho la nchi hiyo Fédération Camerounaise de Football (FECAFOOT)

Najaribu kujiuliza kwa nini FIFA walishindwa kumzuia mchezaji aliyebadilisha uraia wake kutoka kwenye nchi isiyoruhusu uraia pacha?Na Eto'o siyo mchezaji wa kwanza duniani.Lakini naambiwa na wajuzi wa mambo ya uraia

Na hivi karibuni kuliibuka sakata la uhalali wa wachezaji Wacongo

Wachezaji wa DR Congo waliohusika katika kesi hiyo, kama vile Aaron Wan-Bissaka na Axel Tuanzebe, wamekuwa na uraia wa Ulaya au Ufaransa, lakini sheria za Kongo haziruhusu uraia wa pacha. Nigeria inadai kuwa wachezaji hao hawakuwa na sifa za kucheza kwa DR Congo kutokana na sheria hizo ¹ ².

FIFA ikachunguza madai hayo, lakini DR Congo ikakataa malalamiko hayo, ikidai kuwa ni jaribio la "kushinda kupitia mlango wa nyuma"

FIFA walitupilia mbali shauri hilo na moja ya wachezaji aliyepingwa Axel Tuanzebe bao lake ndio limeipeleka DR Congo Kombe la dunia.

Na hapa kwetu lipo sakata la Damaro na ambalo nalo limetupiliwa mbali na wasio halalisha uraia wa mtu kwa maana TFF.

Kuna watu wananiambia hapo kwa Damaro hakuna kitu,kuna propaganda nimebakia kuwashanga.

Hivi wazee wafanye propaganda wakati wanasubiri document halisi iwafikie ili waende CAS!


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons