Rais wa soka Kongo Brazzaville atoroka na kapu la hela

Rais wa Shirikisho la Soka la Congo-Brazzaville (FECOFOOT), Jean-Guy Blaise Mayolas, anatafutwa pamoja na mkewe na mtoto wake baada ya kutoweka,

Mamlaka za Congo-Brazzaville zimewasilisha ombi kwa Interpol ili kutoa hati za kimataifa za kuwakamata,

Mayolas na familia yake walipatikana na hatia ya ubadhirifu wa dola milioni 1.1 za Marekani kutoka FIFA, fedha zilizotolewa kama msaada wa COVID-19 mwezi Februari 2021,

Sehemu ya fedha hizo, dola 500,000, zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya timu ya taifa ya wanawake ya Congo,

Inadaiwa kuwa walikimbia nchi wiki chache kabla ya kusikilizwa kwa kesi yao na wachunguzi wanahisi huenda wanajificha nchini Cameroon au Democratic Republic of the Congo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons