Nyota wa Bomu FC na Ashanti za Ilala, afariki dunia


Mchezaji wa zamani wa Bomu FC, Ashanti FC zote za Ilala, Kumbukumbu FC ya Kinondoni, Agatoni FC ya Mbagala - Mangaya, AFC ya Arusha na MOGO FC ya Majumba 6, Steven Antony Mwaigaga amefariki Dunia jioni ya leo katika hospital ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda ambapo alikuwa amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 6.

Msiba upo nyumbani kwa Baba yake Mzazi eneo la Machimbo Kitunda, taarifa zaidi za mazishi tutawaletea, Mwaigaga ameacha mjane na watoto 2.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.!

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons