MwanaFA uso kwa uso na Mkazuzu wa Clouds FM
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Hamis Mwijuma "MwaFA" amekutana na Mkuu wa Idara ya Michezo Clouds Media Yahaya Mohamedy "Mkazuzu" pamoja na David Mponda Afisa Biashara (Citadel Tanzania Limited) na mbunifu mvumbuzi wa uthaminishwaji wa ligi kuu Tanzania bara na visiwani Zanzibar ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma.
Kikao hicho kilihusisha mazungumzo ya uthaminishwaji wa ligi Kuu na kuingia kwa soka la Tanzania soko la hisa ambapo TFF na DSE wanatarajia kuingia makubaliano siku za karibuni.
Mazungumzo hayo yaligusia pia uanzishwaji wa mfumo wa wachezaji wote Tanzania kuwa na mfuko wao wa uwekezaji kuchangia maendeleo ya wachezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania.
Bwana Mponda pia, ndiye mvumbuzi wa chanzo kipya cha mapato kwa TFF kupitia michezo ya kubashiri (betting) ambapo amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wachezaji na timu za ligi za kuu pamoja na TFF wanaenda kunufaika na sekta hiyo.


