Mbeya City sare sare na Azam FC

TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.

Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 34 katika mchezo wa 18, ikibaki nafasi ya tatu, wakati Mbeya City inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 18 pia, nayo ikibaki nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16.

Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.

Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons