Makonda asimamisha uchaguzi TOC
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesimamisha uchaguzi na uongozi wa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kufuatia malalamiko ya wagombea kuenguliwa bila haki na kukosekana kwa uwazi.
Waziri amesisitiza kuwa uamuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Sura ya 49 ili kulinda utawala wa sheria na maslahi ya umma.
Ili kuziba pengo la uongozi, ameteua Kamati ya Muda itakayoongozwa na Ismail Aden Rage (Mwenyekiti) na Dkt. Steven Mabagala (Makamu Mwenyekiti).
Aidha, kutaundwa kamati ya uchunguzi itakayoshirikisha TAKUKURU na Polisi ili kuchunguza tuhuma za mchakato wa uchaguzi huo na kuchukua hatua stahiki. Waziri amewataka wadau kuwa watulivu wakati Serikali ikirejesha uadilifu ili kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika michezo ya kimataifa.
