Magori asisitiza Mpanzu hajagoma ila anaumwa
“Elie Mpanzu mkataba wake wa sasa utaisha Septemba, kusema anagoma kwa mahitaji ya mkataba mpya ni jambo la ajabu sana.
Kwanza katika wachezaji wana heshima ni Mpanzu na ameumia sana kuikosa mechi ya Azam. Hayo ni maneno ambayo hayana kichwa wala miguu.
Anaumwa lakini anaendelea vizuri na amesafiri na timu kwenda Arusha. Sina uhakika na mechi ya tarehe 9 kama atacheza lakini labda kuanzia tarehe 12.”
“Ilianzia tukapelekwa kuchezwa Zanzibar sababu ya mashindano ya Quran, huko nyuma mashindano yameshawahi kufanyika na baada ya mashindano mchezo ukachezwa. Tuliwauliza wasimamizi wa mashindano ya Quran wakasema wao wanamaliza mapema shughuli zingine zinaweza kuendelea lakini bado mchezo ukapelekwa Zanzibar.”
“Kwanza Loemba hajaletwa na JayRutty, alitafutwa na Kamati ya Usajili kwa kushirikiana na kocha. Mkataba wa JayRutty ndio unasema atasajili mchezaji mmoja ndio tukamwambia alipie gharama zake za usajili. Kwani Mohammed [Dewji] anavyosajili wachezaji kwahiyo ni wachezaji ni wa Mohammed.
Na mkataba wa JayRutty unasema kila mwaka atasajili mchezaji mmoja hivyo na mwakani mjiandae kuna mchezaji mwingine atalipia gharama za kumsajili. Loemba aliumia tangu mechi ya Singida na alianza mazoezi juzi na kocha akamuweka benchi mechi ya Azam.
Hakucheza sababu mwalimu aliona bado timu inayocheza ipo vizuri na hakutaka kuchukua risk ya kumchezesha.”- Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori.
