Loemba aleta mgogoro- wa Jayruthy na Magori
Sakata la Inno Josepin Loemba linaendelea kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Simba SC baada ya kauli tofauti zinazotolewa kuhusu usajili wake.
Ikumbukwe kuwa Jayrutty, ambaye ni mzabuni wa vifaa vya michezo ndani ya klabu hiyo, aliwahi kuwaahidi mashabiki kuwa angechangia kuleta mchezaji mmoja kama sehemu ya mchango wake kwa timu.
Katika mahojiano yake na Crown TV, alieleza wazi kuwa tayari wamemleta Loemba, kauli iliyopokelewa kwa shangwe na mashabiki wengi.
Hata hivyo, kauli za hivi karibuni kutoka kwa Magori zimeleta mkanganyiko baada ya kueleza kuwa Loemba ni usajili wa klabu yenyewe, jambo linaloonekana kupingana na ile ahadi na maelezo ya awali ya Jayrutty.
Hali hii imeacha maswali mengi kwa wadau wa soka: Je, mchango wa mzabuni ulikuwa upi hasa? Na ni kwa nini kuna utofauti wa taarifa juu ya suala nyeti kama hili?
Mashabiki wanahitaji uwazi na kauli moja kutoka kwa uongozi wa Simba SC ili kuondoa sintofahamu hii. Bila kufanya hivyo, maswali yataendelea kuongezeka na kuathiri imani ya wadau juu ya uendeshaji wa klabu.
"Loemba sio mchezaji wa Jayrutty, ni mchezaji ambaye alifanyiwa scouting na Simba kwa kushirikiana na kocha kisha tulimwambia Jayrutty alipie usajili wake kwa sababu Loemba ndo alikuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa.
Kuna makubaliano ya kimkataba kati yetu na yeye ya kulipia usajili wa mchezaji mmoja kila msimu! Sasa kama angemlipia Oura mngesema ni mchezaji wa Jayrutty?"
"Hata mwakani atalipia mchezaji mwingine kama sehemu ya makubaliano ya kimkataba"
- Crescentius Magori (Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba)
