KMC yapokea kichapo kwa Mbeya City

TIMU ya Mbeya City imetoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara
.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Riphat Msuya dakika ya 64, Adili Buha kwa penalti dakika ya 76 na Said Naushad dakika ya 86, wakati ya KMC yamefungwa na Oscar Paulo dakika ya 44 na Juma Shemvuni dakika ya 78.

Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 17 na kusogea nafasi ya 12 kutoka ya 14, wakati KMC inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi zake nane za mechi 17 sasa.

Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.

Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons