Klabu ya Ligi Kuu Burkina Faso yaja kujifunza Young Africans
Timu ya soka ya Usfaburkina kutoka Ouagadougou inayishiriki Ligi Kuu nchini Burkina Faso imewasili makao makuu ya klabu ya Yanga SC kwaajili ya Semina ya Mafunzo ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya mpira wa miguu.
Mafunzo hayo yameanza leo chini ya idara ya Wanachama na Masoko kisha kuendekea kesho kupitia idara nyingine kabla ya kuhitimisha semina hii na kukutana na Rais wa Yanga Eng Hersi Said.









