IJUE ULAYA NA HISTORIA YA KUZAA MADOLA MAKUBWA

Inaandikwa na Fikiri Salum

ULAYA (asili ya jina ni neno la Kiarabu, Wilayaatuni, inaitwa pia Uropa kutoka Kigiriki European ama Ueram jina la Mungu jike Europa) ni bara lililoko katika kaskazini ya dunia likipakana na bahari ya Aktiki upande wa kaskazini, bahari ya Atlantiki upande wa magharibi na bahari ya Mediterranean upande wa kusini.

Mpaka wake wa mashariki kwa kawaida hufafanuliwa kupitia milima ya Uraia, mto Uraia, bahari nyeusi, ingawa mipaka hii ni ya kijiografia na kihistoria zaidi kuliko ya kisiasa.

Kwa eneo la takribani kilomita za mraba milioni 10, 18, Ulaya ni bara dogo la pili baada ya Australia lakini lina idadi kubwa ya watu, ikifikia zaidi ya milioni 750, na yenye msongamano mkubwa wa watu duniani.

Ulaya ina historia ndefu na imechangia pakubwa katika maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kitamadumi duniani, bara hili lina mataifa 44 yanayotambulika kimataifa yakiwemo mataifa makubwa kama Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.

Lakini pia ni pamoja na mataifa madogo kama Vatikani na Liechtenstein, Umoja wa Ulaya (EU) ni moja ya miungano muhimu ya kisiasa na kiuchumi katika bara hili, ikiwa na wanachama 27.

Aidha, Ulaya imekuwa kitovu cha mapinduzi mbalimbali kuanzia mapinduzi ya kitaaluma, na ya viwanda hadi maendeleo ya demokrasia ya kisiasa, na imeendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika masuala ya kimataifa.

UTAWALA

Katika karne ya 20 baada ya vita kuu mbili, nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kushirikiana kwa njia mbalimbali.

BARAZA LA ULAYA LINA NCHI WANACHAMA 47

Mkutano wa usalama na ushirikiano katika Ulaya (Marekani na Kanada ni wanachama pia), Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 28 tangu mwaka 2013.

ULAYA IMEPANGWA KWA UKANDA, INA KANDA NNE

Katika orodha inayofuata KANDA zinatajwa katika utaratibu wa Umoja wa mataifa (UN Categorizations/map).

Lakini utaratibu huo haukubaliki ndani ya Ulaya kwa nchi za Ulaya ya kati, Wajerumani, Waustralia, Waswisi, Wacheki, Waslovakia na Wapoland hukubaliana ya kwamba wenyewe si Ulaya magharibi wala mashariki ila Ulaya ya kati.

Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado kwa mfano suala la Hungaria au Latvia.

NCHI ZA ULAYA

Orodha kamili ya nchi za Ulaya ikitaja ukubwa na mito mkubwa zaidi pamoja na lugha rasmi orodha hii haionyeshi ukanda wa nchi husika, na hii ni idadi kamili ya nchi na mji mkuu wake na kanda zake zote za Ulaya.

ULAYA MASHARIKI

Beralus. Mji mkuu ni Minsk
Bulgaria mji mkuu ni Sofia
Jamhuri ya Czeck mji mkuu Prague
Hungary mji mkuu ni Budapest
Moldova mji mkuu ni Chisinau
Poland mji mkuu ni Warsaw
Romania mji mkuu ni Bucharest
Slovakia mji mkuu ni Bratislava
Russia mji mkuu ni Moscow
Ukraine mji mkuu ni Kiev.

ULAYA KASKAZINI

Denmark mji mkuu ni Copenhagen
Estonia mji mkuu ni Tailinn
Finland mji mkuu ni Helsinki
Iceland mji mkuu ni Reykjavik
Ireland mji mkuu ni Dublin
Latvia mji mkuu ni Riga
Lithuania mji mkuu ni Vilnius
Norway mji mkuu ni Oslo
Sweden mji mkuu ni Stockholm
Uingereza mji mkuu ni London.

ULAYA MAGHARIBI

Austria mji mkuu ni Vienna
Ubelgiji mji mkuu ni Brussels
Ufaransa mji mkuu ni Paris
Ujerumani mji mkuu ni Berlin
Liechtenstein mji mkuu ni Vaduz
Luxembourg mji mkuu ni Luxembourg City
Monaco mji mkuu ni Monaco City
Uholanzi mji mkuu ni Amsterdam
Uswisi mji mkuu ni Born.

ULAYA KUSINI

Albania mji mkuu ni Tirana
Andorra mji mkuu ni Andorra la Veila
Bosnia na Herzegovina mji mkuu ni Sarajevo
Kroatia mji mkuu ni Zagreb
Cyprus mji mkuu ni Nicosia
Ugiriki mji mkuu ni Athens
Italia mji mkuu ni Roma
Malta mji mkuu ni Valletta
Montenegro mji mkuu ni Podgorica
Macedonia kaskazini mji mkuu ni
Skopje
San Marino mji mkuu ni Marino City
Serbia mji mkuu ni Belgrade
Slovenia mji mkuu ni Ljubljana
Hispania mji mkuu ni Madrid
Vatikani mji mkuu ni Vatikani City
Ureno mji mkuu ni Lisbon

MWISHO



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons