Dodoma Jiji yaichakaza Fountain Gate 3-0

TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Airtel Mwigulu mjini Singida.

Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na beki Augustino Nsata dakika ya 38, winga Iddi Kipagwile dakika ya 69 na mshambuliaji Yassin Mgaza dakika ya 90’+1.

Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 18 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 16 za mechi 17 sasa nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16.

Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.

Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons