Damaro aibwaga Simba SC, TFF


TFF imeitupa kesi ya Simba SC dhidi ya Mohamedi Damaro na Yanga SC kama ilivyotarajiwa, baada ya kusikiliza kesi hiyo upande mmoja wa Simba SC pekee.

Hapa chini nimekuwekea hoja za Simba katika kesi hiyo ambayo inategemewa kupelekwa CAS:-

HOJA ZA SIMBA

1. Kanuni za Ligi kuu zinamtambua mchezaji wa Kigeni na Mzawa, hakuna lugha nyingine. Mgeni ni aliyetoka nje ya Tanzania na Mzawa ni Mchezaji wa Kuzaliwa. Damaro anatokea wapi hapo maana hajazaliwa Tanzania.

2. ⁠Kupewa uraia kwa naturalization hakumpi mtu haki zote kama Mzawa, mf. Raia kwa naturalization hawez kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi. Je, kwenye mpira kuna kanuni iliyoruhusu mchezaji ambaye ni raia wa nje kuja kuhesabika ni Mtanzania kwenye Klabu.

3. ⁠Kama Damaro ni Mtanzania, je ana sifa za kucheza timu ya Tanzania au Guinea? Kama hajakidhi matakwa ya kuchezea timu ya Tanzania, maanake kwenye Club ni Mtanzania but National Team ni Guinea. Tanzania lini imeruhusu duo nationality? Hatuoni kwa kiruhusu hili tunavunja sheria za nchi na FIFA?

4. ⁠Fifa imetoa kanuni kuhusu Eligibility (national team) na change of association. Art 7 and 9 (FIFA RGAS na Guidance zake (2021) zimeelezea utaratibu wa kufuata. Art 9 inasema mchezaji hatahesabika kubadilisha association mpaka apate approval ya FIFA.

Kama Damaro hajafanya maombi FIFA na kupata Approval, ni kanuni ipi imetumika kusema ni mtanzania na association yake ni Tanzania.

5. ⁠Damaro FIFA inamtambua raia wa Guinea. Akiuzwa nje ya Tanzania atauzwa kama raia wa Guinea ( isipokuwa kama FIFA imeapprove change of association kuwa Tanzania). Je hatuoni kuwa tunetengeneza mazingira ya uraia pacha kupitia mpira? Madrid wanawatumia Vinicius kama EU players na raia wa spain licha ya TMS kuwatambua kama Brazilian sababu Spain na Brazil zote zina duo nationality, hii haiwezi kutumika kwa nchi isiyo na uraia pacha.

Damaro hajabadili uraia wake FIFA, meaning Tanzania hatuwez kumtumia but Guinea wanaweza kumtumia . Na kwa sheria za FIFA kubadili uraia au association lazima iwe approved na FIFA.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons