Aziz Ki azidi kuwasha moto Libya
Stephanie Azizi Ki leo ameendelea kuonesha makali yake kwenye ligi kuu ya Libya akiwa na klabu yake ya Al-Ittihad SC.
Aziz Ki leo amefanikiwa kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 4-1 walioupata Al-Ittihad dhidi ya klabu ya Shabab Al Ghal kwenye mchezo wa ligi kuu ya Libya.
Hili sasa linakuwa ni goli lake la pili kwenye michezo 6 aliyocheza mpaka sasa ndani ya klabu hiyo kwenye ligi kuu msimu huu.
