Azam FC yaichakaza Fountain Gate 4-0
Klabu ya Azam imetinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA Cup) kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika dimba la Azam Complex, Chamazi kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Wanalambalamba hao wameungana na Simba, Yanga, Coastal Union, JKT Tanzania, TRA United, Singida BS na Mashujaa kwenye hatua hiyo.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Japhte Kitambala dakika ya 15, Abah Abbel dakika ya 21, Ashrafu Kibeku dakika ya 81 na Alobigast Kyobya dakika ya 90.
