Ali Kamwe azua maswali kwa wanahabari

Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC, Ali Shabani Kamwe, ni kama amezua maswali kwa wanahabari kutokana na andiko lake alilolitoa leo.

Nilitegemea mpaka sasa hivi Waandishi wa habari/ Wachambuzi wangekuwa wameshafanya Yafuatayo..

1: Kupiga Simu TFF kuthibitisha kama ni kweli TAASISI HII YA MPIRA NCHINI ndio ilikwenda Uhamiaji na kumuombea URAIA mchezaji Kibu Dennis

2: Kupiga Simu Idara ya Uhamiaji na kuuliza kama Taratibu za Nchi yetu zinaruhusu Taasisi kumuombea Mtu URAIA wa Tanzania kwa sababu ya mpira

3: Nilitegemea warudi tena TFF kuuliza ilikuwaje mchezaji KIBU DENNIS alicheza Ligi Kuu [Mbeya City/ Simba SC] akiwa Binadamu ambaye hana URAIA (FREE STATE). Kanuni Gani ilitumika kuruhusu hili?

4: Nilitegemea Waandishi/Wachambuzi waulize tena WIZARA husika ni kweli Tanzania anaweza kuishi Mtu na akafanya kazi kama mchezaji akiwa HANA URAIA WA TAIFA LOLOTE??


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons