Kocha wa zamani wa Azam FC na ya Tanzania na AS Vita ya DR Congo,Youssouph Dabo raia wa Senegal ameweka wazi nia yake ya kurejea kufundisha soka nchini Tanzania ikiwa tu itatokea klabu ambayo watakubaliana kwenye misingi ya ufanyaji kazi.
Dabo ni kocha mwenye mbinu za kisasa na mwenye kupenda heshima na adabu kwa timu yake.
