Baada ya kufanikiwa timu yake ya Cosmopolitan kufungwa mabao machache dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa hatua ya 32 kombe la CRDB, hatimaye klabu ya Hausing FC ya Njombe inayoshiriki Championship imeamua kumchukua kocha huyo na kuwa kocha wake mkuu.
Seleman Kitunda Simota au maarufu Guardiola, amejiunga rasmi na timu hiyo iliyoweka kambi mkoani Manyara, akizungumza na Mambo Uwanjani Blog, Kitunda amefurahishwa na kujiunga kwake na timu hiyo inayopambania kupanda daraja msimu ujao.
Hausing imeamua kumchukua Kitunda kutokana na uwezo wake aliouonesha dhidi ya Yanga na kuifanya timu hiyo inayoongoza ligi kupata idadi ndogo ya mabao tofauti ikicheza na timu nyingine kubwa ikizitandika idadi kubwa ya mabao.
Katika mchezo huo Yanga dhidi ya Cosmopolitan, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku pia Kitunda anasifika kwa kuwaagiza vijana wake kuoheshimu Yanga na kushambulia kwa mipira ya kushtukiza.
