Leo ndio leo katika uwanja wa New Amaan Stadium, Zanzibar pale watani wa jadi wa soka la Tanzania, Yanga na Simba watakaposhuka uwanjani kuwania pointi tatu muhimu mchezo wa Ligi Kuu bara.
Yanga itakuwa mwenyeji ikiongozwa na kocha wake Pedro Goncalves raia wa Ureno wakati Simba inaongozwa na kocha wake Steve Barker raia wa Afrika Kusini.
Tutegemee mchezo utakuwa mzuri na wa kuvutia, Yanga inataka kuendeleza rekodi yake ya kushinda mbele ya Simba wakati Simba nao wanataka kuhakikisha wanaondoa wimbi la kufungwa na Yanga na ikiwezekana wanapata ushindi ama sare.
