Serikali imetangaza rasmi kuufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia Machi 2026 kwa ajili ya awamu ya mwisho ya ukarabati mkubwa kuelekea AFCON 2027.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amethibitisha kuwa ukarabati huo utachukua kati ya miezi 6 hadi mwaka mmoja, ukilenga zaidi kuboresha:
Eneo la kuchezea (Pitch).
Miundombinu muhimu ya uwanja.
Nini kitatokea?
Hakutakuwa na mechi yoyote itakayochezwa pindi kazi itakapoanza.
Timu zote zitalazimika kutafuta viwanja mbadala kwa mechi za ndani na kimataifa.
Huu ni uamuzi muhimu kuhakikisha Tanzania inatoa burudani ya kiwango cha dunia mwaka 2027
