Mchezaji wa Zamani wa Simba Sc na Sasa Dodoma Jiji “Abdi Banda” baada ya Jana kupewa Adhabu na Bodi ya Ligi ya Kufungiwa michezo (3) na Faini ya Shilingi Millioni 1..
Kwa kosa la kujirusha kwenye Machela kwa nia ya kupoteza muda kwenye mchezo dhidi yao na Simba.
Baada ya kupewa Adhabu Hiyo Banda Ameandika Ujumbe Huu Kupitia Ukurasa Wake wa Instagram:.
“Tumkomoe Mtanga jeuri yule. Mimi bora nirudi kuwa mvuvi au kuangusha nazi tu lkn chuki yangu na nyinyi ni milele.”
“NAOMBENI NISAIDIE PESA YA KULIPA FAINI MAANA MIMI MSHAHARA WANGU LAKI 3.”
(Abdi Banda) Mwaka 2017 Aliandika Ujumbe Huu Kupitia Mtandao wa Instagram Kuwaaga Wanasimba Baada ya Kutoka Kushinda Kombe la Shirikisho Dhidi ya Mbao Fc.
“Ahsante mungu nashukuru kwa hiki ulichotujaalia. Zawadi ya mashabiki wa simba nawaachia acha na mm nitafute maisha sehemu nyingine. Nitamiss vitu vingi hasa sapport yenu na moyo wenu wa uvumilivu ahsanten sana kwaherini“.
NB:
Ikumbukwe Abdi Banda alichezea Klabu ya Simba kwa Mafanikio Lakini Toka Amerudi Kutoka South Africa Ameonekana Kuonyesha Chuki Za Wazi Kwa Klabu yake Ya Zamani Simba Sc.
