BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inatangaza mabadiliko ya uwanja kwa ajili ya mchezo namba 30 wa Ligi Kuu ya NBC, Tanzania Prisons FC dhidi ya Young Africans SC, ambao hapo awali ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya Machi 12, 2026 kuanzia saa 10:00 alasiri.
Mchezo huo sasa utafanyika katika tarehe hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri uliopo jijini Dodoma kuanzia saa 2:00 usiku.
Sababu ya mabadiliko hayo ya uwanja ni uwanja wa Sokoine kufungiwa na Kamati ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Bodi inawatakia maandalizi memo ya mchezo huo wadau wote zikiwemo klabu shiriki.
