Kocha wa Singida Black Stars David Ouma raia wa Kenya, amesema kuelekea mchezo wao na Simba SC kesho jioni katika uwanja wa Airtel uliopo Singida watapata ushindi kwakuwa wanacheza nyumbani.
Tutacheza katika hali iliyo bora zaidi…,” Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma, akielezea maandalizi ya kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba SC.
Amesema kucheza nyumbani ni jambo linalowapa asilimia kubwa ya kushinda mchezo licha ya kukiri kuwa kikosi cha mpinzani wao kimekuwa imara zaidi.
Kwa upande wake goli kipa wa Singida Black Stars Benedict Haule amesema wachezaji wamejiandaa vizuri kutumia mbinu za makocha kuhakikisha wanashinda mchezo huo huku akisema mchezo utakuwa mkubwa kutokana na mpinzani wao.
