Licha ya kucheza ugenini, Simba SC jioni ya leo wamepata ushindi mbele ya wenyeji wao Singida Black Stars katika uwanja wa Airtel uliopo Singida mchezo wa Ligi Kuu bara inayodhaminiwa na NBC.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Anicet Oura dakika ya 06 na Elie Mpanzu dakika ya 86, goli pekee ya Singida Black Stars limefungwa na Mossi Nduwumwe dakika ya 37.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kushikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27 na mechi 12, kesho watani zake Yanga SC watacheza na Tanzania Prisons katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Hata hivyo pambamo hilo lilikuwa na ushindani mkali kwani Singida Black Stars waliikamia Simba na wakitaka kupata ushindi lakini vijana wa Simba nao walikuwa makini na kuibuka na ushindi.
