Kocha mkuu wa CR Belouizdad amefikisha mechi 50 tangu aanze kuifundisha klabu hiyo, akieleza fahari yake kuwa sehemu ya moja ya vilabu vikubwa barani Afrika.
Katika maelezo yake, kocha huyo amesema kuwa ni heshima kubwa kufanya kazi katika klabu hiyo yenye historia kubwa na kuvaa rangi zake kila siku. Ameeleza pia shukrani zake kwa Rais wa klabu kwa kumuamini, pamoja na kujivunia wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wanaopigania nembo ya klabu hiyo kila siku.
Kocha huyo alisisitiza kuwa mafanikio yote wanayoyapata yanawahusu zaidi mashabiki wa klabu hiyo, ambao wamekuwa wakiendelea kutoa sapoti kubwa kwa timu yao.
Ameongeza kuwa sasa amebakiza mechi tano tu kufikia rekodi ya kuwa kocha aliyeiongoza CR Belouizdad katika michezo mingi zaidi mfululizo katika historia ya klabu hiyo ndani ya kipindi kimoja cha kazi. Hii ni hatua muhimu na ya kujivunia kwake binafsi. 📊
Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa kuvunja rekodi pekee hakutoshi, kwani lengo kuu la klabu hiyo kubwa ni kushinda mataji, jambo ambalo linaendelea kuwa kipaumbele kikubwa kwa timu hiyo.
