Kwa mujibu wa Mwandishi Micky, amesema; Rais wa Senegal leo amewasiliana na Dkt. Patrice Motsepe na kumhakikishia kuwa anaungwa mkono kikamilifu katika uongozi wake na kazi anayoifanya ndani ya CAF.
Licha ya Senegal kupeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo CAS, wameweka wazi kuwa Motsepe hakuhusika kwa namna yoyote katika mchakato wa kufanya uamuzi huo, wakisisitiza kuwa hukumu hiyo ilitolewa na chombo huru.
Pia wameeleza kuwa Motsepe hakuwa na mchango wowote katika matokeo ya mwisho ya uamuzi huo.
