Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Congo, Federation Congolaise de Football (FECOFOOT), amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Jean-Guy Blaise Mayolas amepatikana na hatia na mahakama na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa kadhaa yakiwemo utakatishaji wa fedha, kughushi nyaraka, mgongano wa kimaslahi kinyume cha sheria, na ubadhirifu wa fedha za FIFA wakati wa kipindi cha janga la COVID-19.
Fedha hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa wanawake na ujenzi wa kituo cha mafunzo (training center), lakini inadaiwa zilitumika vibaya.
Mke wake na mwanawe pia wamepatikana na hatia katika kesi hiyo.
Viongozi wawili wa shirikisho wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
