Huu ni msafara wa wachezaji wa klabu ya Pyramids FC wakiwa safarini hapo jana wakielekea Morocco kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya AS FAR katika CAF Champions League.
Kama kawaida yao, klabu imeandaa ndege maalum (private jet) yenye viti vya Business Class kwa ajili ya timu nzima, ili kuhakikisha wanapata faraja na maandalizi bora kabisa kabla ya mchezo wao wa robo fainali.
Mchezo utapigwa siku ya March 13 kwenye uwanja wa Prince Moulaye Abdellah jijini Rabat na itakuwa ni kwenye majira ya saa 4 usiku kwa saa za Morocco ambapo ni sawa na saa 7 usiku kwa saa za Tanzania.



