Inaandikwa na Fikiri Salum
Ilipoishia
SAFARI YA KWENDA NCHI YA AHADI
KUT 12:29-42 inasimulia Waisrael wote walivyokimbia Misri pamoja na mifugo yao waliposikia mayowe kutoka nyumba za majirani wao wote.
Endelea.
Katika safari yao wakaongozwa na Mungu kwa sura ya wingu mchana na ya moto usiku (KUT 13;17-22; Yoh 8;12): hivyo Mungu alionesha wazi kuwa hawaachi hata kidogo bali anawashughulikia kwa namna tofauti kadiri ya mahitaji.
KUT 14;5-31 inasimulia jinsi Wamisri, kisha kuwalilia wafu wao, walianza kuwatafuta Waisrael kwa Farao na magari wakawakuta karibu na bahari ya Shamu.
Lakini Waisrael walivuka bahari kama kwamba ni nchi kavu, kwa kuwa maji yamegawanyika, kumbe Wamisri wakazama kwa kuwa maji yamerudi mahari pake (EB 11;29) asubuhi Waisrael wakaona maiti za Wamisri wote zikielea, wakamshangilia Mungu aliyewaokoa.
(KUT 15:1-21 inatuletea wimbo ambao maneno yake ni kati ya yale ya kale zaidi katika biblia) , hivyo Mungu aliwaokoa tena watu wake katika maji na huu pia ni mfano wa ubatizo ambao unaadhimishwa hasa usiku wa Pasaka.
Hata katika hatari ya kukandamizwa Mungu alidai Waisrael watulie kwa imani ya kuwa ushindi ni wake tu, tena walitakiwa wasiyasahau kamwe mang' amuzi hayu, kwa kuwa ndiyo msingi wa imani ya dini yao.
Sisi vile vile tunatakiwa kukumbuka daima ubatizo wetu ambapo Mungu ameutoa, baada ya ushindi wa Pasaka safari ikaendelea mpaka kufikia nchi aliyoahidi Mungu, ila Waisrael wakaja kusahau uwezo wake na kumlalamikia kipumbavu hata kumchosha, KUT 10;1-11 inatuonya tusifanye vile.
Kama kawaida malalamiko ya kwanza yalihusu kula na kunywa (KUT 15;22-17-7) Mungu aliwakubalia kwa kuwaletelemshia Kwale halafu maana hasa chakula hicho kiliwashangaza Waisrael wakazidi kukikumbuka hata wakamdai Yesu awapatie tena kama kweli ndiye Musa mpya.
Yesu akawajibu kuwa mwenyewe ndiye chakula cha uzima kutoka mbinguni kinachotulisha safarini hapa (Yoh 6;23-59), vilevile kuhusu maji, Mungu alijitokeza katika mwamba huko Masa au Meriba, lakini alichukizwa sana na matendo (EB 3:15-19).
Shida nyingine ya kawaida kwa makabila ya wahamiaji ni kupigana vita Waisrael walilazimika kufanya hivyo na Waamaleki, wakapata ushindi si kwa nguvu zao, ila kutokana na sala ya Musa, mwombezi wao (KUT 17;8-16), sisi taifa la Mungu tunatakiwa tutegemee Sala kuliko uhodati wetu na daima tuwe na watu wenye kumwinulia Mungu mikono yao kama Musa Jangwani.
AGANO LA MLIMA SINAI
Walipofika mlima huo wa kutisha, Mungu alimuita Musa aupande Ili aseme naye, huku wengine wakibaki chini, hapo akampa Musa masharti ya agano lake na Waisrael (KUT 19) Akiwa muumba na hasa mkombozi wao alidai waishi kitakatifu kwa kushika amri kumi, ambazo tatu zinahusu heshima kwake na saba uhusiano na watu wengine (KUT 20;2-17)
Ndiyo mawe mawili ambayo Musa alipewa halafu Yesu akayakamilisha katika amri kuu ya upendo kwa Mungu na Kwa jirani (MK 12:28-34) amri hizo zinaweza kujulikana na kukubaliwa na mtu yeyote mwenye mapenzi mema.
Lakini Mungu alipenda kutusaidia tujue kwa urahisi na hakika zaidi tufanye nini Ili kumpendeza, tuwe watu wake naye awe Mungu wetu kweli kweli, Agano hilo upande wa Mungu ni imara kwa kuwa yeye ni mwaminifu kabisa, shida Iko upande wetu tulip geugeu, tukiahidi tusitekeleze, ndiyo sababu likahitajika agano lingine lililofungishwa na Yesu Kristo (2 Tim 2;11-13).
NDAMA WA DHAHABU
KUT 32 inatusimulia uasi wa Waisrael ulivyofikia kilele chake walipojitengezea Mungu wa dhahabu mwenye sura ya fahari (Biblia kwa dharau inasema "Ndama" na mla nyasi).
Hata Haruni alikubali kufuata matakwa yao huku mdogo wake akichelewa mlimani (Mdo 7;38-42) Israel kuabudu ndama ilikuwa chukizo mbele ya Mungu, kwa kuwa Mungu hana mbadala wa yeye kufanyiwa ibada.
INAENDELEA
