Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Nabi ndiye kocha aliyeleta mabadiliko makubwa Yanga

Anaandika Musa Mwakisu

Nasreddine Nabi ndiye kocha aliyeleta mabadiliko makubwa ya uchezaji ndani ya klabu ya Yanga SC.

Haikuwa kazi rahisi kwake kwasababu wapo ambao walikuwa hawamuelewi na kuna muda kibarua chake kilikuwa kinashikiliwa na utandu wa buibui,ila imani yake juu ya filosofia yake ilimbeba sana.

Makocha wengi wamepita na kutengeneza filosofia zao kama babu Hans van der Pluijm,lakin mwalimu Nabi alikuja kuiamsha Yanga kwa njia zake.

Na kuitengenezea ubora mkubwa sana uwanjani,kila mchezaji anayeanza na anayekaa benchi wanakupa ubora ulele.

Zipo mechi nyingi sana ambazo Yanga SC walicheza kwa ubora na ujivuni wa hali ya juu kutokana na maarifa ya Nabi.

Leo nimesoma taarifa ya klabu ikisema kuwa kwenye tathimini yao ya michezo ya mzunguko wa kwanza,licha ya kufanya vizuri kwenye baadhi ya takwimu ila wamegundua kuna changamoto inayoifanya timu icheze soka tofauti na ile iliyozoeleka.

Ukiona mazingira kama hayo yanaelezwa kupitia barua rasmi ya klabu,bila shaka kuna shida kwenye benchi la ufundi kushindwa kuendana na filosofia ya klabu.

Mwalimu Nabi hana timu kwa sasa baada ya kuachana na Kaizer Chiefs,na ilisemwa wakati anaachana na timu hiyo ya Afrika ya Kusini aliamua kuwa karibu na mke wake aliyekuwa mgonjwa.

Bila ya kumvunjia heshima kocha Pedro Gonçalves hiki kilichoandikwa kwenye taarifa kwa umma,na kurejeshwa kwa Moalin inawezekana ikawa ni taa nyekundu au ya kijani.

Ila kilicho muhimu kama mambo hayatakwenda sawa,itakuwa ni wakati wa kufikiria kumrejesha baba wa filosofia ya Yanga SC kwa miaka ya hivi karibu kocha Nasreddine Nabi,ingawa cv ya kufundisha Afrika ya Kusini imempelekea kuwa kocha mwenye kuhitajika kulipwa pesa nyingi.

Bila shaka kwa bwanyenye GSM inaweza kuwa sio shida.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe