Wakati mvutano kati ya Israel, Marekani na Iran ukiendelea huko Mashariki ya Kati, mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameondoka kutoka Riyadh, Saudi Arabia na kuelekea, Hispania huku wafuasi wake na mashabiki duniani kote wakionesha wasiwasi kuhusu usalama wa nyota huyo na familia yake.
Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or aliruka kutoka Jijini Riyadh alipokuwa akiishi tangu alipojiunga na klabu ya Al-Nassr FC kwenda Madrid, Uhispania akitumia ndege yake binafsi usiku wa manane wakati Jiji hilo likikabiliwa na mashambulizi ya anga huku ndege zisizo na rubani zikiripotiwa kulenga ubalozi wa Marekani Nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa za ufuatiliaji wa safari za ndege, ndege binafsi ya Ronaldo aina ya Bombardier Global Express 6500 iliondoka Riyadh majira ya saa 8:00 usiku na kuwasili Madrid majira ya saa 1:00 asubuhi, ikipitia anga la Misri na Bahari ya Mediterania kabla ya kutua Hispania.
