Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MWANZO WA AFRIKA

Inaandikwa na Fikiri Salum

HISTORIA ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote, kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani hasa Ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbalimbali, na simulizi au hekaya za mapokeo.

Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi za hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithibati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia.

Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.

HISTORIA YA AFRIKA

Hapo kale, bara la Afrika lilishuhudia matukio mengi ya harakati za mwanadamu kuliko mabara mengine ya ulimwenguni.

Wataalamu wa athali wamegundua athali za Zamadamu zinarudi nyuma kufikia hadi miaka ya milioni nne, na athali za ustaarabu wa Wamisri wa kale huko Misri na Wafoinike huko Tunis na sehemu nyinginezo za Afrika kaskazini katika karne ya 9 KK.

Harakati za madola makubwa ya Wazungu na Waarabu ziliweza kuonekana kabla ya karne ya 4 BK, na Waarabu walianza kuingia Afrika huko Habasha (Ethiopia) tangu karne ya 7 BK na kutangaza dini ya Uislamu na kueneza katika maeneo mbalimbali ya Afrika pamoja na kuanzisha biashara na ustaarabu na kuimarisha mamlaka zao katika Sudan ya wakati huo tangu karne ya 8 baada ya Kristo.

Himaya- za Ghana, Mali na Songhai zilikuwa zikijulikana kwa utajiri mkubwa na biashara stawi, iliyokuwa ikifanyika wakati huo ya dhahabu na bidhaa nyinginezo.

Mwisho wa karne ya 15 BK, himaya ya Songhai ilikuwa na nguvu kuweza kuita chini ya utawala wake mamlaka ya Mali, sehemu nyingine za kusini mwa Afrika zilikuwa wakati huu hazijulikani sana, na historia yake ilikuwa bado haijadajiliwa.

Baina ya karne ya 1 KK na karne ya 16 BK watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbalimbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijiji, mashamba na mamlaka katika sehemu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo.

Maeneo mengine ni Zaluba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wa wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu, ndipo walipoanzisha mamlaka zao za Bunyoro, Buganda, Rwanda na Ankole.

UKOLONI

Wazungu walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe