Mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya TRA United vs Simba SC iliyopangwa kuchezwa leo saa 10:00 jioni, imeahirishwa kutokana hali ya uwanja iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jijini Arusha.
Mechi hiyo sasa itapangiwa siku nyingine, Simba ilitakiwa kucheza leo Ili kufikisha mechi 13 sawa na wenzake Yanga, Azam FC na Singida Black Stars ambao wana viporo.

