Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MTU MWEUSI NA OIDUVAI GORGE

Inaandikwa na Fikiri Salum

BONDE la Oltupai (maarufu kwa Kiingereza kama Olduvai Gorge) ni eneo la Kiakiojia linalopatikana katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania ambalo ni kati ya yale muhimu zaidi duniani.

Bonde hilo lipo katika hifadhi ya Ngorongoro na karibu na Ile mbuga ya Serengeti, ni mahari ambapo Zamadamu, viumbe wa kale waliokaribiana na mwili wa binadamu, waliishi tangu miaka milioni 2 hivi iliyopita.

Kwa kuwa watu wanadhaniwa kutokana nao, eneo hilo pengine limeitwa kwa Kiingereza Craile of manking, kitovu cha binadamu, ambako wameishi katika eneo hilo kwa walau miaka 17, 000 mfululizo.

Katika eneo hili Mwanaakiolojia Mary Leakey ndipo alipogundua fuvu la kichwa la kiumbe wa kale wa jamii hiyo.

Pamoja na mabaki ya mifupa ya Tembo, Kongoo wenye pembe kubwa na Mbuni, tarehe 17 Julia 1959 aligundua mabaki ya fuvu la kichwa la Pararthropus Boisei (pamoja na mumewe alimwita kwanza zinjanthropus) ambalo lipo katika makumbusho ya Dar es Salaam.

Huyo anadhaniwa kuwa mtangulizi wa binadamu wa sasa, karibu na Olduvai Gorge kilomita 95 kusini kwake, kuna eneo la Laetoli ambapo mwaka 1972 huyo huyo Mary Leakey aligundua nyayo za kale miaka (milioni 3. 7 iliyopita) za Zamadamu waliotembea kwa miguu miwili.

MWISHO 



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe