Mwalimu wa soka kutoka nchini Afrika Kusini, Rulani Mokwena, amehitimisha rasmi safari yake na klabu ya MC Alger ya nchini Algeria kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Baada ya kuachana na klabu hiyo, ripoti za uhakika zinaeleza kuwa kocha huyo sasa anatarajiwa kuelekea nchini Libya kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa klabu ya Al Ittihad.
Hatua hiyo inamfanya Mokwena kwenda kuungana na wachezaji wake wa zamani, Thembinkosi Lorch na fundi wa mpira Stephane Aziz Ki, ambao tayari wapo nchini humo wakitumikia klabu hiyo.
Muunganiko huu unatazamwa kama "reunion" ya kiufundi inayoweza kuifanya Al Ittihad kuwa tishio kubwa, kwani Mokwena anajua vyema jinsi ya kuwatumia nyota hao wawili waliowahi kung'ara chini ya mikono yake huko nyuma.
