Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MJUE NABII IBRAHIM- 2

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia

Mwa 22: 1-19 inatuletea habari ya kusisimua kuhusu sadaka ambayo Mungu alimdai Abraham yaani kumchinja Isaka, ni kimoja kati ya vielezo vya imani ya binadamu, imani inayooneshwa kwa matendo ya utiifu (Yak 2:21-22).

Endelea

Abraham hakusita kumrudishia Mungu kile alichopewa, akaondoka alfajiri akasafiri mpaka mahari alipoambiwa (Wayahudi) wanaamini mlima huo ndipo walipojenga hekalu la Yerusalem) kwa niaba ya waamini wote, Abraham alikuwa tayari kumchinjia Mungu mwanae pekee ampendaye.

Lakini kadiri ya Injili atakayemtoa kweli mwana pekee ni Mungu baba (Yoh 8-16) Yesu ndiye mwanakondoo aliyeuliziwa na Isaka na ambaye Mungu akajipatia juu ya mlima Kalivari alioupanda huku amejitwika kuni, basi mti wa msalaba.

Abraham aliamini uwezo wa Mungu juu ya mauti na hasa uaminifu wake kwa ahadi alizompa kwa hiyo akarudishiwa mwana hai kama mfano wa ufufuko, na katika yeye, yaani katika mzawa wake watu wote wakabarikiwa


Maisha ya imani yanadai daima sadaka, hasa ya mambo yanayopendwa zaidi (Rom 12:1-2) ndiyo njia ya kujaliwa baraka zinazopitia ubinadamu wetu.

Mwa 24 inasimulia kirefu jinsi Abraham kabla hajafa alivyomfanyia mpango wa ndoa Isaka kufuatana na mila zao, ila alikataa kabisa asirudi kwao, bali kwa vyovyote abaki katika nchi Ile aliyoahidiwa na Mungu.

Hivyo imani izidivkuongoza uzao wake kama ilivyomuongoza mwenyewe, Isaka akawa mrithi wa Abraham watoto 12 wa mwanaye Yakobo ni chanzo cha makabila 12 wa Israel hivyo Abraham huangaliwa pia kama Babu wa Wayahudi wote na Waarabu pia.

SALA YAKE (MWA 8:27)

"Nimeshika kusema na bwana Mimi ni mavumbi na majivu tu".

IBRAHIMU KATIKA KURANI

Hasa katika Uislamu Abraham (Ibrahimu) ni kielelezo muhimu cha imani kwenye Kurani hutajwa mara kwa mara katika sura 25 na mistari 245, kwa jumla habari zake zimekuwa tofauti na taarifa za biblia lakini heshima inalingana.

Habari zinazosimuliwa katika biblia juu ya Isaka babu wa Israel pengine hurudia kwenye Kurani na kutafsiriwa na wengi kuwa zilimuhusu Ismael kaka yake na babu wa Waarabu, anaaminiwa kuwa alijenga Kaaba kama msikiti.

MWISHO

Endelea kutazama Mambo Uwanjani Blog kesho kutakuwa na stori nyingine kali na ya kusisimua 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe