TIMU ya Mashujaa FC imelazimishwa sare ya kudungana bao 1-1 na Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Beki Nyenyezi Shaaban alianza kuifungia Mashujaa FC dakika ya 55, kabla ya Sadick Ramadhani ‘Immobile’ kuisawazishia Fountain Gate dakika ya 90’+4.
Kwa matokeo hayo, Mashujaa FC inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 11 ikiizidi pointi mbili Fountain Gate baada ya timu zote kucheza mechi 16 hadi sasa.
