Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUUMBWA KWA DUNIA

Inaandikwa na Fikiri Salum

DUNIA (kutoka neno la Kiarabu) wakati mwingine pia Ardhi na Kwa neno la asili la Kibantu nchi, ni Gimba la angani ambapo juu yake tunaishi sisi binadamu na viumbe hai wengine wengi, tukipata mahitaji yetu, kuanzia hewa ya kutufaa na maji.

Dunia ni mojawapo ya sayari zinazoelea katika anga la ulimwengu, kuna sayari nane zinazolizunguka jua, dunia yetu ikiwa sayari ya tatu katika mfumo wa juavna sayari zake.

Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kizio Astronomia 1, dunia huchukua siku 365, 256 kulizunguka jua, na masaa 23,9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756.

Dunia huwa na mwezi mmoja 1.

Umri wa dunia hukadiriwa kuwa na miaka bilioni 4,5 (1/2)

Ni mahari pekee katika ulimwengu panapojulikana kuna uhai ulioaminiwa kuanza miaka bilioni 3.5, hivi iliyopita, uhai unapatikana kwa spishi milioni 10-14 za viumbe hai pamoja na  wanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7, 2 (4).

UMBO LA DUNIA

Umbo la dunia linafanana na tufe au mpira unaozunguka kwenye mhimili wake, mhimili wa dunia ni mstari kati ya nchi zake.

Lakini si tufe kamili, ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta, ilihali umbali kati ya ncha mbili ni kilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume ikweta ni km 12, 756.

Yaani kipenyo hivi kinazidi takribani kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha, tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia, kwani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi.

Kwa hiyo mahari duniani palipo karibu zaidi na anga la nje si mlima Everest kwenye Himalaya bali mlima Chimborazo nchini Ecuador (5).

Kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani nchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii.

Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maneno yake.

Kwa jumla dunia ni sayari pekee katika mfumo wa jua yenye maji katika hali ya Kiowevu usoni mwake, asilimia 96, 5 ya maji yote yaliyopo duniani, maji ya bahari huwa na asilimia 3, 5 chumvi ndani yake.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe