Mchambuzi nguli wa soka nchini, Edo Kumwembe Edo Kumwembe ametoa tathmini yake juu ya mwenendo wa kocha mkuu wa Young Africans, Pedro Gonçalves, akibainisha kuwa kocha huyo amekuwa akipitia milima na mabonde tangu awasili klabuni hapo.
Kumwembe ameeleza kuwa uteuzi wa viungo wanne wenye sifa zinazofanana uwanjani umekuwa ukirudisha nyuma makali ya timu hiyo katika kushambulia.
Katika uchambuzi wake, Edo Kumwembe {@edokumwembe } amefafanua mbinu hizo kwa kusema:
"Kocha Pedro Gonçalves amekuwa na milima na mabonde tangu awasili, kwa kucheza na viungo wanne wanaofanana, Duke Abuya, Mudathir, Damaro na Maxi Nzingeli aliyekuwa anashinda katikati ilikuwa kama vile anacheza na 'handbrake'.
Wazungu huwa wanasema hivyo kwa kocha ambaye anaangalia zaidi namna ya kujihami kuliko kupeleka mashambuliaji mbele."
