Kocha wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo George Lwandamina amesema mchezo wa kirafiki dhidi ya Argentina utakuwa mgumu lakini wamejiandaa kupambana vizuri na kuleta ushindani wa hali ya juu.
Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo katika chuo kikuu cha Lusaka, Lwandamina alisema kucheza na mabingwa hao wa dunia itakuwa kazi kubwa.
Chipolopolo watakuwa ugenini nchini Argentina Machi 31 mjini Buenos Aires katika mechi ya kihistoria ya kirafiki ambayo inawakutanisha Zambia dhidi ya mabingwa hao wa dunia.
Hata hivyo wachezaji wakubwa hawakuweza kujumuishwa katika kikosi hicho cha timu ya taifa kutokana na majukumu kwenye timu zao.
