Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KANISA KATOLIKI NA HISTORIA YAKE

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia

Katika juhudi hizo Monasteri za Wabenedikto na Wamisionari waliotumwa katika Ulaya nzima walitoa mchango mkubwa, pamoja na ule wa Karolo mkuu, mfalme wa Wafaranki kabila la Kijerumanik muhimu zaidi katika historia, ambalo lilikuwa la kwanza kuingia kanisa katoliki moja kwa moja bila kupitia Ukristo na Kiario.

Endelea

KATOLO alitawazwa na Papa Leo 111 kuwa Kaisari wa magharibi (800), ushirikiano kati ya mapapa na makaisari wa Dola takatifu la Kiroma (Ujerumani wa leo na nchi kando kando) ulikuwa na mafanikio kadhaa na matatizo mengi zaidi na zaidi.

Baada ya Uislamu kuanza katika Karne ya 7 na kuteka maneno mengi ya Kikristo, kanisa katoliki liliona wajibu wake kuitikia maombi ya Wakristo waliohitaji msaada dhidi ya dhuluma iliyolenga kuwafanya wasilimu, ndiyo chanzo cha vita ya msalaba vilivyotawala karne zilizofuata.

Wengi wanaoma karne ya 13 kuwa kilele cha matunda ya kanisa katoliki katika kulea upya Ulaya magharibi kwa kuzaa hasa mashirikia ya ombaomba ya Fransisko wa Asizi na Dominikp Guzman, mitindo mipya ya sanaa, pamoja na vyuo vikuu walipostawi walimu wa kanisa kama Thoma wa Akwino na Bonaventura.

Utaifa uliotokea Ulaya magharibi kuanzia ufalme wa Ufaransa katika karne ya 14 ulivuruga umoja wa kanisa kiasi kwamba kwanza mapapa waliishi Avignan, mbali na Roma, kwa miaka 69 (1309-1378) halafu kwa miaka 38 (1378-1409) kukawa na farakano la kanisa la magharibi, waamini mengine waliomfuata Papa wa Roma na wengine Antipapa wa Avignon wakidhani ndiye Papa wa kweli.

Mambo hayo na makwazo mengine yaliwafanya wengi wadai bila mafanikio urekebishp wa kanisa tangu karne za nyuma, hatimaye yalichangia katika karne ya 16 ustawi wa matengenezo ya Kiprotestanti ambayo yalitenga na Papa sehemu kubwa ya Ulaya Kaskazini na kuvunjikavunjika katika madhehebu mengi.

Hapo juhudi za urekebisho wa Kikatoliki ziliongezeka na kuleta hali mpya hasa baada ya mtaguso wa Trento (1545-1563).

Kabla ya hapo, uvumbuzi wa njia za baharini za kufikia Amerika (1492), bara lililokuwa halijulikani na Wakristo, na Asia mashariki, ulichochea upya umisionari.

Kwa kuwa nchi zilizoshika kasi kwa kiasi kikubwa maneno mapya ya duniani kote wakati huo zilikuwa za Kikatoliki (Hispania na Ureno), kanisa kwa kutumia hasa mashirika ya kitawa uliweza kufidia upungufu uliosababishwa na Uprotestanti.

Upinzani dhidi yake uliojitokeza katika matengenezo hayo, ulizidi kupata nguvu katika zama za mwangaza ba mapinduzi ya Kifaransa (Karne ya 18) halafu katika ukoministi ulioenea kutoka Urusi hadi therusi moja ya dunia (Karne ya 20) na kuwa Wakatoliki milioni kadhaa (mbali na Waorhodoski wengi zaidi).

Mbele ya changamoto hizo mtaguso wa pili wa Vaticano (1962-1965) ulielekeza njia mpya za kuendeleza Ukristo katika ulimwengu wa kisasa.

Kwa mtazamo wa imani, historia hiyo yote inaonesha upande mmoja udhaifu na ukosefu wa Wakatoliki hata katika ngazi za juu, Mungu wa kuleta watakatifu wapya katika mazingira yoyote.

MWISHO


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe