Inaandikwa na Fikiri Salum
KANISA katoliki likiwa la zamani (Waorthodoksi) na Waorthodoksi wa mashariki wanashiriki sifa hiyo) na kubwa kuliko madhehebu yote ya Ukristo, historia yake inashika sehemu muhimu ya historia ya kanisa lote duniani tangu lilipoanza mwaka 30 hivi BK hadi leo.
Baada ya Yesu Kristo kuhubiri na kukusanya wafuasi kati ya Wayahudi wa Karne ya 1 hao walitumwa naye duniani kote, hasa wanaume 12 aliowaita mitume "yaani walitumwa".
Waandamizi wao katika uongozi wa kanisa walianza kuitwa maaskofu, na kati ya yule wa Roma alizidi kushika nafasi ya pekee kwa sababu mtume Petro alifia dini katika mji huo kutokana na dhuluma dhidi ya Ukristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero (mwaka 64) na kuendelea kwa kwikwi hadi ilipokomeshwa na Kaisari Konstantino mkuu aliyetangaza huko Milano Uhuru wa dini kwa wananchi wote (313).
Dhuluma haikufaulu kuzuia uenezi wa dini hiyo mpya katika Dola la Roma, mwishoni mwa karne ya 2, maaskafu walianza kukusanyika katika sinadi Ili kuamua kuhusu masuala ya imani nk, mwaka 325 Konstantino aliitisha huko Nisea (Uturuki) mtaguso mkuu wa kwanza wa maaskafu wote Ili kurudisha umoja wa kanisa uliovurugwa na uzushi wa Ario kuhusu Yesu Kristo.
Mwaka 380 Kaisari Theodostus 1 alifanya Ukristo wa Kikatoliki kuwa dini rasmi ya Dola hilo kubwa lililoendelea kwa namna tofauti mashariki na magharibi kwa karne nyingi zilizofuata.
Ushindi huo ulifanya wengi watamani vyeo ndani ya kanisa, kwa kuwa viliendana sana na heshima na mali, hivyo ubora ulipungua, kabla yake Armenia ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama dini ya taifa (301).
Ushindani kati ya majimbo makuu muhimu zaidi (Roma, Konstanhopoli, Aleksandria, Antiokio na Yerusalemu) ulisababidha mafarakano makuu (431,451,1054) yaliyoacha kanisa katoliki katika Ulaya magharibi karibu peke yake.
Huko, katika fujo iliyosababishwa na makabila yasiyostaaribika ya Wagermanik walioteka maneno yote ya magharibi, lilichukua jukumu la kuokoa ustaarabu wa Ugiriki wa kale na Roma ya kale uliokwisha athiriwa na Ukristo kwa kiasi kikubwa.
Katika juhudi hizo, Monasteri za Wabenedikto na Wamisionari waliotumwa katika Ulaya nzima walitoa mchango mkubwa, mfalme wa Wafaranki, kabila la Kijerumanik muhimu zaidi katika historia, ambayo lilikuwa la kwanza kuingia kanisa katoliki moja kwa moja bila kupitia Ukristo wa Kiario.
INAENDELEA
