Beki wa klabu ya Young Africans Sports Club, Dickson Job, leo asubuhi amefanyiwa upasuaji uliofanikiwa nchini South Africa kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Simba Sports Club.
Job alipata majeraha wakati wa mchezo huo na kushindwa kuendelea kuumaliza uwanjani.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amesema nahodha huyo amefanyiwa operesheni asubuhi ya leo na kwa mujibu wa madaktari hali yake inaendelea vizuri.
“Nahodha wetu Dickson Job amefanyiwa operesheni asubuhi ya leo nchini Afrika Kusini na Alhamdulillah jambo limekwenda vizuri kabisa,” amesema Kamwe.
Mashabiki na wanachama wa Yanga pamoja na Watanzania kwa ujumla wamemtakia nafuu ya haraka beki huyo muhimu wa timu hiyo anayefahamika kwa umahiri wake mkubwa uwanjani.
