Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Inno Loemba, ameanza kuonja matunda ya kazi yake baada ya kukabidhiwa gari jipya aina ya Toyota Crown. Zawadi hiyo imetolewa na kampuni ya JAYRUTTY Investment, ambao ndio wazabuni rasmi wa jezi na vifaa vyote vya michezo vya klabu ya Simba SC.
Hili ni mwanzo tu wa neema kwa wachezaji wa Simba, kwani JAYRUTTY imepanga kutoa magari mengine kwa nyota Libasse Gueye, Anicet Oura na Djibrilla Kassali.
