Kocha mkuu wa timu ya Azam FC ya Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Florent Ibenge raia wa DR Congo, ameigwaya Yanga SC ambao atakutana nao kesho katika uwanja wa Mkapa.
"Huu mchezo tulipaswa tucheze Chamazi, Tutacheza mechi zote mbili uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ni uwanja wa nyumbani wa Yanga na Simba, Yanga Wana nafasi ya kushinda kwasababu wapo nyumbani ila hatulalamiki, tutacheza na kujaribu kushinda"
Frolent Ibenge, Kocha Mkuu Azam FC.
