Inaandikwa na Fikiri Salum
Ilipoishia jana.
KITENDO chenyewe alichokiazimia kuifanya mara mbili zote hizo na mwenyezi Mungu akamfadhi nacho ni kutaka kukesha katika ngoma za Arusi mbili za marafiki zake waliooa katika mji wa Makkah.
Endelea.
Lakini Mungu alimpa usingizi mkubwa katika masiku yote hayo mawili hata hakuweza kufumbua jicho, wala kunyanyua miguu kwenda mahari, hajapata kuudhuria hata mara moja katika ibada za kuabudu sanamu wala kula chakula kilichochinjwa kwa ajili yao, moyo wake ulichukizwa na hayo na mambo mengine yaliyo mabaya.
Tangu udogo wake mtume alipndokea na sifa nzuri ambazo hapana hata mtu mmoja katika hirimu zake aliyekuwa nazo zote, kila sifa zinazohesabiwa kuwa ni njema na ndizo alizokuwa nazo tangu utoto wake.
Mkewe Aisha alipoombwa kutaja kidogo sifa za mtume, alisema hivi, "sifa zake ni zile sifa nzuri zinazosofiwa na kurani na katika kurani zimetajwa chungu ya sifa zilizo nzuri.
Mtume mara nyingi alikuwa akisema sikupata kufanya hata siku moja yale mambo waliyokuwa wakiyafanya makafiri", kwa hivyo yeye hakupata kuabudu sanamu, kulewa, kuzini, kucheza kamari wala hakumdhurumu mtu kitu chake na kama haya.
Lakini alikuwa msemakweli, mwaminifu, mpole na mwenye haya na sifa nyingi nyinginezo bora kama hizi, watu wa Makkah walikuwa wakimsifu kwa tabia zake, hata wakampa jina la Muhammad Al Amin (mwaminifu) alikuwa hatajikani ila kwa jina la Al Amin.
Wakubwa na wadogo walikuwa wakimheshimu na kumpa amana zao kuwawekea, hata baada ya utume.
KABLA YA KUPEWA UTUME
Makureshi ni watu wa biashara, kila kureshi alipata kufanya kazi hii. safari moja baadhi yao walipokuwa wakienda Yemen katika biashara zao, baba yake mdogo wa pili bwana Zubeyr alimshauri ikiwa atapenda kusafiri, mtume aliridhia akaenda naye mpaka Yemen, wakakaa huko muda wa siku tatu tu kisha wakarejea, wakati huo mtume alikuwa mtoto wa miaka 9.
Hata alipotimia miaka 12 mwaka 582, alisafiri tena pamoja na baba yake mdogo mwingine, bwana Abu Talib.
INAENDELEA
