FIFA imeidhinisha mabadiliko kadhaa ya Sheria ambayo yataanza kutumika kwenye Kombe la Dunia 2026:
Wachezaji watakaobadilishwa wana sekunde 10 kuondoka uwanjani. Wakichelewa, mchezaji anayeingia atalazimika kusubiri dakika moja kabla ya kuingia.
Mipira iliyokwenda nje itakuwa inafanywa ndani ya sekunde 5, la sivyo mpira utapelekwa upande wa pili.
Wachezaji wanaopata matibabu watalazimika kuondoka uwanjani na kusubiri dakika moja kabla ya kurudi Uwanjani.
VAR sasa itaruhusiwa kuingilia kati kwenye kadi za njano za pili (Kadi nyekundu) na kwenye mipira ya kona kama kuna kosa la wazi la kiamuzi.
