Mshambuliaji wa timu ya JKT Tanzania, Edward Songo, amesema kwamba mchezo wa mpira wa miguu umempa ajira kwenye Jeshi la Kujenga Taifa, JKT na anajivunia kucheza soka akiwa muajiriwa wa jeshi hilo.
Akizungumza na Sports Extra ya Clouds FM, Songo aliyeibukia vilabu vya Majimaji FC na JKT Mlale zote za mkoani Ruvuma, amesema kujituma na kuwa na nidhamu nzuri vimepelekea yeye kunyakuliwa na JKT Tanzania na baadaye muajiriwa.
Amewaasa vijana wenye vipaji kama yeye kuzingatia nidhamu na kujituma kwani yeye anafurahia mafanikio aliyonayo sasa.
